1 Thessalonians 5:2-7

2 akwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. 3 bWakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.

4 cBali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. 5 dNinyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku. 6 eKwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi. 7 fKwa kuwa wote walalao hulala usiku na wale walewao hulewa usiku.
Copyright information for SwhKC